Makamu wa Rais Ndejembi aungana na wananchi kufanya mazoezi Coco Beach

 


Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Septemba 19, 2026, ameungana na wananchi mbalimbali kufanya mazoezi ya asubuhi katika eneo la fukwe za Coco Beach, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ndejembi amefanya mazoezi hayo katika njia ya kutoka Coco Beach kuelekea Daraja la Tanzanite, akishiriki pamoja na wananchi waliokuwa wakifanya shughuli za mazoezi katika eneo hilo.

Mazoezi ya pamoja kama hayo yameendelea kuwa sehemu ya shughuli zinazowakutanisha wananchi katika kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kuzingatia afya ya mwili.

Post a Comment

Previous Post Next Post