Na Carlos Claudio, Dodoma.
Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) katika jitihada zake za kuifikisha Nishati yake ya Rafiki Briquettes kwa makundi mbalimabli ya Watanzania, leo tarehe 22 Septemba 2026, imebisha hodi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT) kwa kuwapa mafunzo na kuwahamasisha wajumbe hawa kuungana na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza agenda ya Nishati Safi ili kufikia 2034 matumizi ya Nishati Safi kwa Watanzania yawe yamefikia angalau asilimi a 80.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa White House Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Baraza kuu la UWT pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa UWT kutoka Wilaya zote Tanzania.
Akitoa mafunzo hayo, Meneja wa Masoko na Mahusiano ya Umma kutoka STAMICO bwn Deus Alex Ntukamazina amewaelezea wajumbe hawa ufanisi wa Nishati hiii katika kuwaka muda mrefu, umuhimu wake katika kulinda mazingira na afya za watu, matumizi yake katika matumizi ya nyumbani kama kupika chakula, kuchoma nyama,kuchemsha vitu mbalimbali pamoja na matumizi ya viwandani kama kukausha mazao na kutoa Nishati ya Joto kwa ajili ya kuyeyusha vitu mbalimbali
Bwn Ntukamazina amewaelezea pia kuhisiana na fursa ya biashara ambayo wajumbe hao wanaweza shirikiana na Shirika kisambaza Nishati hii na kujipatia kipato.
Ameongeza kuwa Nishati hii ni salama kwa sababu imethibitishwa na Shirila la Viwango Nchini TBS na pia Shirika linatumia mitambo maalumu ( Carbinizer) ambayo hupunguza joto la Nishati hii kuepuka kutoboa masufuria pamoja na kupunguza hewa za ukaa na hewa nyingine ambazo sio rafiki kwa Mwili wa Mwanadamu.
Wajumbe mbalimbali waliopata nafasi ya kuongea na kuuliza maswali wameiomba STAMICO ifanye mafunzo kama haya sehemu mbalimbali nchini huku wakionesha shauku ya kutaka kuwa mawakala na wakiahidi kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha matumizi ya Nishati hii Safi ambayo ni mbadala sahihi wa kuni na Mkaa
Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mhe Mary Chatanda(MCC) amewataka wajumbe hao kuchangamkia fursa hii ya kuwa wasambazaji wa Nishati hii nchi nzima lakini pia wamuunge mkono Mkt wao wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye yeye ndio muasisi wa Agenda ya Matumizi ya Nishati Safi na kinara wa masuala yote ya kulinda Mazingira Afrika nzima.
STAMICO, imedhamiria kuendelea kwa kasi kuisambaza Nishati hii Safi ili kuunga juhudi za Mhe Rais kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi na Salama katika azma ya kulinda mazingira na afya za Watanzania


Post a Comment