Kairuki azindua programu ya mitaji kwa start-up za TEHAMA


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema ubunifu wa kiteknolojia ni nyenzo muhimu katika kuongeza tija, kuanzisha biashara mpya, kutengeneza ajira na kukuza uchumi katika zama za teknolojia.

Kairuki ameyasema hayo leo Oktoba 2, 2026 jijini Dodoma akizindua programu ya kuwezesha mitaji kwa kampuni changa za TEHAMA (Start-ups).

Kairuki amesema kuwa kwa kutambua umuhimu huo, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeweka mkazo katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kama kichocheo cha kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa.

"Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza ubunifu kupitia taasisi ikiwemo Tume ya TEHAMA na Tume ya Sayansi na Teknolojia, sambamba na kuimarisha ujuzi na uwezo wa kitaifa katika sekta hiyo,"amesema.

Amesema lengo ni kuhakikisha mawazo mazuri ya Watanzania hayaishii kuwa mawazo pekee, bali yanapata mazingira ya kuyabadilisha kuwa bidhaa, huduma au biashara zinazoweza kukua na hatimaye kuanzisha kampuni zenye ushindani katika soko la kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya tume ya TEHAMA Dkt. Henry Mwanyika amesema kwa muda mrefu kampuni changa zilikuwa zinakwama katikati kutoka na kukosa mitaji lakini ujio wa progaramu kama hiyo kutasaidia na kwenda kutatua changamoto hiyo na kuziwezesha kampuni changa kushindana ndani na nje ya nchi.

"Program hii inaenda sambamba na dira ya tume ya Tehama na taifa ya 2050, sisi kama tume ni daraja la kuwasaidia vijana kabla na baada ambapo prigramu hii itaenda kusaidia kukuza uchumi na ajira kwa vijana,"amesema

Pia amesema mkopo na sio ruzuku hivyo kila shilingi inabidi kurudishwa kwaajuli ya kwenda kufungua fursa kwa vijana wengie.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Status Association, Zahoro Muhaji amesema takribani Shilingi trilioni moja zimeelekezwa katika uwekezaji kwenye kampuni changa za TEHAMA (Start-ups) nchini Tanzania tangu mwaka 2021, hatua inayotajwa kuchochea ukuaji wa sekta hiyo na kuibua fursa zaidi kwa vijana na wabunifu wa teknolojia.

"Mitaji tunayopewa kupitia programu hii si sadaka wala ruzuku, hivyo wanufaika tunapaswa kuhakikisha inatumika kwa tija na kurejeshwa ili kutoa fursa kwa kampuni nyingine changa kunufaika,"amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post