Na Carlos Claudio, Dodoma
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Mark Kihula, ameonya kuhusu madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na lumbesa, akisema kubeba mzigo unaozidi kilo 105 kunaweza kusababisha madhara kwa mbebaji katika miaka inayofuata.
Kihula amesema hayo leo, Septemba 18, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO kuhusu utekelezaji wa shughuli za WMA kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na mwelekeo wa 2026/2027.
Amesema matumizi ya lumbesa yamepungua kwa kiasi kikubwa, ingawa bado hayajaisha kabisa, huku WMA ikiendelea kutoa elimu na kusimamia matumizi sahihi ya vipimo.
Ameeleza kuwa lumbesa haiwezi kutambuliwa kwa kuangalia mzigo kwa macho pekee, bali lazima upimwe, na mzigo unaozidi kilo 105 ndio unaotajwa kuwa lumbesa.
Aidha, amewataka wafanyabiashara katika masoko kuacha kuuza mazao kwa kuangalia gunia badala ya kutumia mizani na kutoza kwa kilo, akisema matumizi sahihi ya mizani yanaongeza uwazi na usawa katika

Post a Comment