Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeandaa bonanza la michezo katika Viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma, kwa lengo la kuimarisha mshikamano, ushirikiano na mahusiano mazuri miongoni mwa watumishi wake.
Bonanza hilo lilihusisha michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, kushika kuku, kukimbia ndani ya magunia pamoja na mbio za kubeba yai kwenye kijiko, iliyoongeza burudani na hamasa kwa washiriki.
Katika mchezo wa mpira wa miguu kwa wanaume, timu za Biashara na Utawala na Vitengo na Ufundi zilitoka sare ya mabao 2-2. Kwa upande wa netiboli, timu ya Biashara na Utawala iliibuka na ushindi wa mabao 7-5 dhidi ya timu ya Vitengo na Ufundi.
Bonanza hilo lilishirikisha pia Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, aliyeshiriki pamoja na watumishi wengine katika michezo hiyo.
Kupitia bonanza hilo, DUWASA inaendelea kuhamasisha michezo kama njia ya kujenga afya bora, kuongeza ari ya kazi na kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wake.





Post a Comment